Friday, 28 April 2017

TAKUKURU PWANI YAPOKEA MALALAMIKO 363





Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond mapema leo amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha julai 2016 hadi march 2017.  Amesema Takukuru bado inaendele ana mapambano ya Rushwa na kwa sasa mafanikio makubwa yanaonekana huku kukiwa na kesi 4 ambazo zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali, aidha takukuru imefanikiwa kupokea jumla ya malalamiko 363 kati ya hayo malalamiko 252 yanahusishwa na rushwa na uchunguzi wake unaendelea huku malalamiko 98 hayahusiani na vitendo vya rushwa. aidha kamanda wa takukuru mkoa a Pwani ameendelea kuwaomba wakazi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na takukuru katika kutoa taarifa zitakazo fanikisha kupatikana kwa watoa na wapokea rushwa.

No comments:

Post a Comment