Friday, 31 March 2017

RIDHIWANI AWATULIZA WAPIGA KULA WAKE WA MIONO NA SAADANI.




























Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani kikwete Jana alijikuta katika wakati mgumu wa kuwatuliza wapiga kula wake wa Jimbo la chalinze katika kata ya Miono wakati wananchi hao walipo funga barabara kwa lengo la kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Munguungano Mh Kassim Majaliwa wakati akipita Eneo hilo kwenda Hifadhi ya Wanyama Saadani.

wananchi hao walifunga barabara kwa lengo la kutaka kumuelezea waziri mkuu tatizo la kuwepo kwa Mgogoro wa wakulima na wafugaji ambao wamekuwa wakisababisha uvunjifu wa amani.

Mhe Ridhiwani aliwataka wananchi hao kutulia ili kufikisha ujumbe wao kwa waziri hatua hiyo ilichukua muda hadi wananchi waho kutulia na kutoa ujumbe wao uliongozwa na diwani wa kata ya miono Juma Mpwimbwi ambae alisema kata hiyo imekuwa na upungufu wa chakula, ukosefu wa maji na kero kubwa ni mgogoro wa wakulimana na wafugaji.

hata hivyo waziri mkuu waliwaahidi serikali yake kusimamia na kutatua kero zote zinazo wasumbua wananchi na kumuagiza mkuu wa Mkoa kuwenda kwenye kata hiyo kuchunguza tuhuma za mkuu wa kituo cha polisi Miono na hakimu wa mahakama ya mwanzo ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji na hivyo kuwaonea wakulima pindi wanapo fikishwa katika vituo hivyo vya kupata haki.




No comments:

Post a Comment