Mbunge wa jimbo la Mtama mheshimiwa Nape Moses Nauye amelazimika kutoa chozi baada ya kutakiwa kupita juu kwa kuwakanyaga wakina mama waliokuwa wamelala chini kama njia moja wapo ya kutimiza mila za kusini
amesema tendo hilo lilimpa wakati mgumu sana na hata kushangaa chozi likimtoka kwani hakuwa ametegemea kufanyiwa jambo kama hilo,
akizungumza katika ukurasa wake wa twita Nape amesema kwa Mila za kusini endo hilo ni la kiheshima na kama angekataa angeonekana kuwa ana dharau sana.
zoezi hilo limetokea hivi karibuni wakati mbunge huyo alipofika jimboni kwake kuzungumza na wapiga kula wake.

No comments:
Post a Comment