Timu ya soka ya
Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1
katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka
wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana ikawa
ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo wa leo
Simba wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni wakiwa
na pointi 56 baada ya michezo 25.
katika mchezo
huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba
wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa
bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph Huku
bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi
kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi
cha pili.
Kwa matokoe
hayo yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya
pointi 56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar
wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam
wenye pointi 44.
No comments:
Post a Comment