Mbunge wa jimbo la
Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akionyesha mifuko ya saruji 500
aliyochangiwa na wadau mbalimbali ili kusaidia katika ujenzi wa uzio wa
kituo cha afya Mlandizi,
Mbunge wa jimbo la
Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akishiriki nguvu kazi na baadhi ya wananchi
katika uzinduzi rasmi wa ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi
.(picha na Mwamvu Mwinyi)
WADAU na viongozi
mbalimbali jimbo la Kibaha Vijijini,wamejitokeza kumuunga mkono mbunge
wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa kufanikisha ujenzi wa uzio wa kituo cha afya
Mlandizi.
Ujenzi huo unatarajiwa
kugharimu mil. 200 na ukikamilika utaondoa kero hiyo iliyodumu miaka
mingi . Jumaa aliyasema hayo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi huo
ambapo hivi karibuni alianza kwa kuweka alama ya msingi.
Alieleza kwamba,
wameshakubaliana na wananchi na wenyeviti wa vitongozi 26 kuwa kila
kitongoji kitachangia sh.240,000 . “Madiwani kila mmoja atachangia
240,000 hivyo wanatarajia kukusanya zaidi ya sh. mil.4, mfuko wa jimbo
sh. mil. 4 kununulia tofali zitakazoanzia ujenzi”alisema .
Hata hivyo,tayari wadau
wamemkabidhi mifuko 500 ya saruji iliyogharimu sh. mil. 6, kokoto tani 7
kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, nondo tani moja
sh. mil. 3.6.
Jumaa alisema ,kwa
msingi kero ya ukosefu wa uzio ni kubwa inayosababisha usumbufu kwa
wagonjwa kutokana na watu,pikipiki kupita na kupiga kelele.
Alieleza kuwa ujenzi huo
utafanyika kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza unatarajia kutumia
zaidi ya sh. mil. 40. Baada ya uchimbaji wa msingi itafuata kumimina
zege kisha kuanza ujenzi wa tofali na awamu hiyo itachukua wiki mbili.
Jumaa alisema hadi sasa
ni juhudi za mbunge na wafadhili ambazo wanategemea kuanza ukuta wa
mbele, kuchimba msingi na kumwaga zege . “Tumezindua rasmi ujenzi ,lengo
ni kutekeleza moja ya vigezo vya kituo chetu kupanda hadhi ya hospitali
ya wilaya”
Alitaja vigezo
vinavyotakiwa kuwa ni pamoja na kuwepo kwa chumba cha upasuaji na
kuhifadhia maiti ,kuongeza watumishi wa afya, madaktari na kigezo
kikubwa ni ujenzi wa ukuta.
Jumaa alisema, kwa sasa
amejipanga kwenda sambamba na kauli mbiu yake ya “Sisi kwanza serikali
baadae “. Anawaomba wadau wa afya na serikali kuendelea kumuunga mkono
ili tatizo hilo libakie historia.
Mbunge huyo alimshukuru
makamu wa Rais mama Samia Suluhu kwa kuahidi kushirikiana nae kujenga
uzio huo. Diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala alimpongeza Jumaa
kwa kuanzisha suala hilo na kusema kwa muda mrefu kituo hicho kilikuwa
kikipata usumbufu.
Makamu Mwenyekiti
Godfrey Mwafulilwa alisema walipokea wazo la ujenzi kutoka kwa mbunge
huyo kwenye kikao ambapo alishauri kwenye mpango wa mwaka 2016/2017
halmashauri iangalie namna ya kuchangia.
Tatu Jalala Mwenyekiti
wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlandizi alisema wamekubaliana kila
mwenyekiti wa Mji huo atachangia sh.240,000 kwa ajili ya ujenzi huo

No comments:
Post a Comment