Monday, 10 April 2017

MBUNGE WA RUFIJI ALIA NA UBOVU WA BARABARA YA NYAMWAGE HADI UTETE

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mkoani Pwani tarehe 8 April 2017, amefanya ziara ya kujionea ubovu wa Barabara ya kuelekea Halmashauri ya wilaya, Makao Makuu ya Wilaya Utete baada tuu ya kuingia Nchini. 
  
Amesema Barabara hiyo ni mbovu na haifai, "tuwakumbushe wananchi kuwa, nimeikumbusha serikali mara nyingi sana kuhusu ubovu wa Barabara hii katika kila kikao cha Bunge kuliko Mbunge yeyote, Mbunge wa CCM wa aina yangu ya Uchapa kazi, iwapo nitashindwa kulisimamia Jambo, ni Ngumu sana kwa Mtu mwengine kuliweza, kwa maana, jukumu nililokabidhiwa na wananchi ninalitendea Haki ipasavyo kwa mapenzi ya Chama changu, mapenzi ya Warufiji wote bila kujali itikadi zao" 

Amesema Tarehe 3March.mwaka huu alitumia nafasi ya kuzungumza na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "juu ya vitu nilivyomuomba ni Barabara ya Nyamwage -Utete, pamoja na Ikwiriri-Mwaseni 96km, alituahidi Ikwiriri tarehe 3, kuwa ataanza na Nyamwage Utete, 33km kabla ya 2020 iwe imekamilika. Tuendelee kumuombea Afya Njema Rais wetu aweze kutekeleza ahadi hii" mheshimiwa  mbunge ameongeza kuwa maumivu haya ni ya wanarufiji wote, huduma za Afya kuelekea Hospitali yetu ya wilaya ni sawa na hakuna kwasasa; sababu karibu ya 70% ya wananchi wote wa RUFIJI,wanaishi Nje ya Makao makuu ya wilaya Utete, 


 Hali ni Mbaya; Ambulance haiwezi tembea mwendo wa kasi kuwaisha mgonjwa, hata ikitokea dharura huwezi kuiwahi. Mwendo wa Km 33 huweza kuchukua mpaka 2-4hrs barabara ikiharibika zaidi.
Ninaimani na Rais wangu Magufuli, Ninaimani kilio cha Warufiji kimepata suluhisho.. mheshimiwa Mohamedi Mchengerwa ameyasema hayo pamoja na mambo mengine ya kuhimiza maendereo na kutembelea miradi mbalimbali kubwa ni kujionea usumbufu wanao upata watumiaji wa barabara ya Nyamwage - Utete.

No comments:

Post a Comment